The 5th International CHAUKIDU Conference KAMPALA, Uganda

Main Topic: The Worldwide Development of Kiswahili and the Sustainability of Other African Languages

Venue: Kampala – Kyambogo University, Kampala, Uganda 

Date: December 13- 15, 2019 (Saturday & Sunday)

Workshop: December 13, 2019 (Friday)

Workshop Topic: Experiences and Methods of Teaching Kiswahili 

Arrival: Thursday, December 12, 2019

Target Audience: All Kiswahili stakeholders around the world

The fact that Swahili is one of the wider languages of communication (lingua francae) in the East and Central Africa region is a matter that does not need to be debated. However, the fact that lingua francae are accompanied by benefits and challenges or that they positively or negatively affect some communities is a claim that has raised a strong debate within and outside the academia. This is an ongoing debate that calls for responses.

In response to this debate, the 5th International CHAUKIDU Conference aims to provide an opportunity to explore and reflect deeply on the relationship between the development of Kiswahili and the prosperity or underdevelopment of other African languages in the East African region. By doing so, this forum will have made a significant contribution to the broader discussion which could ultimately have an important impact on academic, policy, social, and even attitudinal issues on the daily life of members of the East African community and elsewhere in the world.

Alongside the above goal, the 5th International CHAUKIDU Conference to be held in Kampala – Uganda, will bring together various Kiswahili stakeholders around the world to discuss the development of Kiswahili alongside other East African languages. It is our expectation that many Kiswahili stakeholders will be able to discuss and contribute to these issues through presentations, and talks. We also hope that these discussions will stimulate the development of our prestigious Kiswahili language as well as the other African languages spoken in and outside East Africa.

In conclusion, the conference will provide opportunities for both lovers and Kiswahili advocates, teachers, students, researchers, journalists, politicians, artists, curriculum developers, language officials, publishers, scientists, traders, etc., to exchange and to share among other things, knowledge, expertise, and professionalism related to Kiswahili language.

SUB TOPICS/ PANELS

 • Kiswahili and politics/administration/ leadership (safety and security, migration, diplomacy, )
 • Kiswahili and culture (traditional, religious beliefs, sports, and cultural constructs.)
 • Kiswahili and economic development (industrial, agricultural, fishing, tourism, mining, infrastructure etc)
 • Kiswahili and education (educational levels, the language of instruction/learning, academics, research, publication etc)
 • Kiswahili and the Arts (music, drama/film, animated, )
 • Kiswahili and literature (theory, oral, written, poetry, fiction, )
 • Kiswahili and Linguistics (morphology, Syntax, theory, )
 • Kiswahili and other African languages (how they build and complement each other, etc.),
 • Kiswahili and the media (television, social networks, blogs, )
 • Kiswahili for speakers of other languages (Africa, Europe, Asia, America, etc.)
 • Kiswahili and its dialects (colloquial Swahili, Sheng and Kiswanglish, etc.)
 • Kiswahili, technology and globalization
 • Kiswahili and sensitization, spread (knowledge, ideology, technology, etc.)
 • Kiswahili and cooperative societies and their development
 • Kiswahili studies and research

The deadline for receiving abstracts: 31st May 2019 Please submit your abstract before the deadline to chaukidu2019UG@gmail.com

Notification for accepted abstracts: 15th July 2019

Deadline for submission of full papers: 30th September 2019

 Conference Fees:

 1. Participants from East Africa: $ 00
 2. Participants from other parts of Africa: $ 00
 3. All students: $ 00
 4. Participants from outside Africa: $ 00

 Register before 30th  September 2019 to save on the fees!

Download: 

CHAUKIDU Conference Kampala 2019 EngREV

Kongamano la Kampala 2019ENGREV (1)

Kongamano la Kimataifa la Tano la CHAUKIDU KAMPALA, Uganda

 MADA KUU: Ukuaji wa Kiswahili Duniani na Ustawi wa Lugha Nyingine za Kiafrika

 MAHALI: Kampala– Chuo Kikuu cha Kyambogo, Kampala Uganda

TAREHE: Desemba 13- 15, 2019 (Jumamosi & Jumapili)

Warsha: Desemba 13, 2019 (Ijumaa)

Mada: Uzoefu na Mbinu za Ufundishaji wa Kiswahili Kuwasili – Alhamisi Desemba 12, 2019

WASHIRIKI / WALENGWA: Wadau wote wa Kiswahili duniani kote

Hoja ya kwamba Kiswahili ni mojawapo ya lugha za mawasiliano mapana (lingua francas) katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati, ni suala ambalo halihitaji mjadala. Hata hivyo, kwamba lingua francas huambatana na faida na hasara au huwa na athari chanya

na hasi katika jamii husika, ni madai ambayo yameibua mjadala mkali ndani na nje ya wigo wa kiakademia duniani kote. Mjadala huu uko hai, unaendelea na unataka majibu.

Mintaarafu mjadala huu, Kongamano la tano la kimataifa la CHAUKIDU linalenga kutoa fursa ya kuvinjari na kutafakari kwa kina kuhusu uhusiano uliopo kati ya ukuaji wa Kiswahili na ustawi au uviaji (udumazaji) wa lugha nyingine za Kiafrika katika ukanda wa Afrika ya mashariki. Kwa kufanya hivi, Kongamano hili litakuwa limetoa mchango mkubwa katika mjadala mpana ambao hatimaye matokeo yake yanaweza kuwa na manufaa ya kitaaluma, kisera, kijamii, na hata kimtazamo katika maisha ya kila siku ya wanajamii wa Afrika ya Mashariki. na kwingineko duniani.

Sambamba na lengo hilo hapo juu, Kongamano la tano la kimataifa la CHAUKIDU litakalofanyika jijini Kampala, nchini Uganda linalenga kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wa Kiswahili duniani kote ili kujadili uendelezaji na unawirishaji wa Kiswahili na lugha nyingine za Afrika Mashariki. Ni matarajio yetu kuwa wadau wengi wa Kiswahili watachangamkia fursa ya kujadili na kuchangia masuala haya kupitia mawasilisho, na mazungumzo na pia ni matumaini yetu kuwa mijadala hii itachochea uendelezaji wa lugha yetu adhimu ya Kiswahili pamoja na lugha zetu nyingi zinazozungumzwa katika eneo la Afrika ya Mashariki na Kati.

Kwa kuhitimisha, Kongamano hilo litawapa fursa wapenzi na wakereketwa wa Kiswahili, walimu, wanafunzi, watafiti, waandishi, wanahabari, wanasiasa, wasanii, wakuzaji wa mitaala, maafisa wa lugha, wachapishaji, wanasayansi, wafanyabiashara, n.k., kubadilishana na kuelimishana kuhusu maarifa, weledi, tajiriba, taaluma n.k. zinazohusiana na lugha ya Kiswahili.

MADA NDOGO/MAJOPO

 Kiswahili na siasa/utawala/uongozi (usalama, ulinzi, uhamiaji, diplomasia, nk)

Kiswahili na utamaduni (jadi, imani za kidini, michezo, ujenzi, mavazi, vyakula, mapishi, nk) Kiswahili na uchumi (biashara, viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii, madini, miundombinu) Kiswahili na elimu (ngazi za elimu, lugha ya kufundishia/kujifunzia, taaluma, tafiti, uchapishaji) Kiswahili na Sanaa (muziki, maigizo/filamu, vibonzo, nk)

Kiswahili na fasihi (nadharia, simulizi, andishi, riwaya, ushairi, tamthiliya, nk)

Kiswahili na isimu (maumbo, miundo, nadharia, nk)

Kiswahili na lugha za Kiafrika (kujengana, kukamilishana, nk) Kiswahili na upashaji habari (magazeti, vijarida, redio, runinga, mitandao ya kijamii, blogu, nk) Kiswahili kwa wageni (Afrika, Ulaya, Asia, Amerika, nk

Kiswahili na lahaja zake (Kiswahili cha mitaani, kiSheng, kiSwanglish, nk.) Kiswahili na teknolojia na utandawazi

Kiswahili na uhamasishaji, uenezi (maarifa, itikadi, teknolojia, nk) Kiswahili na vyama vya ushirika na maendeleo yake

Utafiti wa Kiswahili na taaluma zake

Tarehe ya mwisho kupokea ikisiri: tarehe 31 Mei, 2019 Tafadhalini tumeni ikisiri zenu kabla ya tarehe ya makataa kwa: chaukidu2019UG@gmail.com

Tangazo la ikisiri zilizokubaliwa: tarehe 15 Julai, 2019

Tarehe ya makataa ya miswada kamili ya makala: tarehe 30 Septemba 2019

Ada za kushiriki:

 1. Washiriki kutoka Afrika Mashariki: $40.00
 2. Washiriki kutoka sehemu nyingine Afrika: $50.00
 3. Wanafunzi wote : $20.00
 4. Washiriki kutoka nje ya Afrika: $150.00

Jisajili mapema kabla ya tarehe 30 Septemba 2019 na huenda ukaokoa kiasi fulani cha ada!

Download: 

CHAUKIDU Conference Kampala 2019 EngREV

Kongamano la Kampala 2019ENGREV (1)